Sunday, 4 August 2013

Majanga - Snura




Chombezo
Mo fire gal (Sauti ya kiume)

Beti 1
Mama yuko hoi mama tumpeleke hospitali,  Dokta anataka salary,
‘Pigwa nimepigwa mie, polisi kawai yeye,  kibao megeuziwa miye,
Mama yuko hoi mama tumpeleke hospitali, Dokta anataka salary,
‘Pigwa nimepigwa mie, polisi kawai yeye,  kibao megeuziwa miye,
Pombe nimenunua mie, kulewa kalewa yeye ugomvi kaanzisha yeye
Kijijini nimtoe mie, kumlisha nimlishe mie, jeuri afanye yeye
Pombe nimenunua mie, kulewa kalewa yeye ugomvi kaanzisha yeye
Kijijini nimtoe mie, kumlisha nimlishe mie, jeuri afanye yeye

Kiitikio
Majanga, majanga mbona majanga  x2

Majanga (Mbona mbonaaaaa) x3

Beti 2
Ndoa tumefunga sie mapenzi yetu wenyewe talaka udai wewe,
Nyimbo nimeimba mie, video nimeshuti mie, shoo ukafanye wewe,
Ndoa tumefunga sie, mapenzi yetu wenyewe, talaka udai wewe,
Nyimbo nimeimba mie video nimeshuti mie, shoo ukafanye wewe
Chumba nitafute mie, kodi nilipe mwenyewe, nje unilaze wewe
Gari ninunue mie, mafuta niweke, mie misele upige wewe
Chumba nitafute mie, kodi nilipe mwenyewe, nje unilaze wewe
Gari ninunue mie mafuta niweke mie misele upige wewe

Kiitikio
Majanga, majanga mbona majangaaaa x2

Majanga (Mbona mbonaaaaa) x3

Beti 3
Kumzaa nimzae mie, kumlea nimlee mi, matusi anitukane yeyee
Mahari atoe yeye, kuoa aoe yeye, vya ndani uvile wewe
Kumzaa nimzae mie, kumlea nimlee mi, matusi anitukane yeyee
Mahari atoe yeye, kuoa aoe yeye, vya ndani uvile wewe
Hela katafuta yeye, nyumba kajenga mwenyewe mali tugonmee sie,
Kufiwa nifiwe mie, kulia nilie mie pole uchukue wewe
Hela katafuta yeye, nyumba kajenga mwenyewe mali tugonmee sie,
Kufiwa nifiwe mie, kulia nilie mie pole uchukue wewe

Kiitikio
Majanga, majanga mbona majangaaaa x2

Majanga (Mbona mbonaaaaa) x3

Tuesday, 14 May 2013

Karibu Dar - Kara Jeremiah ft Ben Paul


Utangulizi
Dada tuma eeh! Ngoja kwanza,
Producer mbezi
Yo ha haaaa  0444

Ubeti wa 1
Picha linaanza kama muvi ya Solomoni,
Gafla vumbi linazidi wajanja wanavaa miwani,
Hii ndio dar karibu ili usijisikie nyumbani,
Hapo Ubungo usinunue simu utauziwa sabuni,
Panda daladala tukutane buguruni,
 kuna watu wanapiga ndole utadhania majini
Gizani usiku utaona  rangi zote za bikini,
wanauza mwili ili wanunue wali maini,
usicheke broo! Kwa sababu mi sio Mr. Bean,
chunga wallet hapa kuna wizi wa mfukoni,
haukawii kushuka kwenye gari hauna phone,
kuwa makini uvukapo huku gari hazipigi honi,
dala dala zinaa,Bajaj zinakesha macho,
 Kama huamini ngoja siku ije uamini we Tomaso,
Wasio na kazi wanashindia stori za freemason,
Wajanja wamepanga sinza, Kino na Tabata,
Mchana wanazibua vyoo usiku wanakula bata,
Usikojoe ovyo bro! Mgambo watakukamata,
Hii ndio dar, mbona unadata  kabla hata hujapata starter?

Kiitikio x 2
Mmh bata ni daily, daily’
Karibu bushman kaa chini tukupashe habari
Shangaa mataa Dar ugongwe na gari (Dar es salaam ya sasa)

Ubeti wa pili
Karibu sana kwenye hili jiji la joto,
Uswahilini chumba kimoja baba mama na watoto,
Si ulisikiaga mabomu ya gongo la mboto?
Yalifanya rafiki yangu wa damu akafia Ghetto,
Yaliacha kovu kubwa kama la mbagala,
Dar es salaam watu wengi tu hawanaga pa kulala,
Kama unataka mirungi twen’ zetu mitaa ya ilala,
Magomeni, mi ujanja wangu wote niliitwa fala,
 Watu wanaingiza pesa wakiwa wamelala,
Watu wengi toka waje hawajawahi kurudi kwao,
Sababu hawana nauli japo wamemisi ndugu zao,
Kuhusu kushinda na njaa hapa ndo zao,
Wauza sura wanaishi kwa kuuza mademu zao,
Mama anauza bangi, Baba amekata ringi anashinda anacheza bao,
Wake zao wanazini kulisha watoto wao,
Vijana wao wanatembeza karanga, wanatembeza maji,wanatembeza vocha,
Jioni wanakabidhi hesabu kwa bosi wao,
Hii ndio dar, ukipenda unaweza kuiita bongo,
Machizi wakikosa hela ya bia wanakula gongo,
See, haiwi siri uswahilini ukipata mchongo,
Wapangaji watakuandama bro mpaka utahama,
Ni majungu mixer wanga, utaenda tu kwa mganga, U
tapo lala Ghetto kwako kasha ukamwagiwa mchanga

Kiitikio x 2
Mmh bata ni daily, daily’
Karibu bushman kaa chini tukupashe habari
Shangaa mataa Dar ugongwe na gari (Dar es salaam ya sasa)

Ubeti wa tatu
Dar es salaam ingekuwa nchi, huku Rais angekuwa Lowasa
Huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa,
Usione watu wamependeza, wengine hawana hata mia,
Hapa mboga ni maharage, nyanya chungu na bamia,
Brother man anatembea toka keko kwa miguu,
Anakwenda mlimani city kununua mkate tu,
(Are you on the facebook?) Ndo maswali ya maduu,
Ukitaka demu wa peke yako kata mgomba lala juu,
Ukimwita demu wako bar wanakuja crew,
Utachunwa mpaka ubaki na raba ubaki miguu juu,
Hapa bomba halijatoa maji mwezi mzima,
Hii ni uswahilini tu na sio kwa jiji zima,
Twende Mbezi au Masaki yanatoka mwaka mzima,
Katiza Kwa Mtogole uporwe simu mchana,
Siku hizi mwanaume anavaa suruali ya kubanaa,
Siku hizi dada’ko anakalio za kichina, ukimtafuta humpati
Ameshakuwa wa kimjinimjini.



Monday, 22 April 2013

Kubum Kubam - Niki wa Pili



Intro.
Yeah, it’s river baby, Nako to Nako baby,
Daz Knowledge (Daz knowledge) the Aaa city dream
Let’s go

Ubeti 1
Hii michano sio muchano kina rabadaba
Punchline kama vyumba kwenye maktaba,
Na break kama news get ready kwenye TV,
Na break ma injury bila news wala GV, nipo na Daz Knowledge
Pen and paper it’s time to get college,
Sinukii pafyumu wala sinuki jasho,
Nani anafyum uswazi hakuna mipasho
Kuna mererani, ngome jela na uraiani, pembe tatu za maisha
R back Tangara be KRS one and siwezi be careless one,
Kama kufanya sifanyi matusi, kama kuchana nachana sichani ku diss
Watumishi watakatifu wanawatumishi ma bodyguard,
na vibaka wanalindwa na hirizi za jadi,
 unapanda mbegu juu ya mbegu eti kisa nyapara?

Kiitikio x 2
Nani anafyum uswazi hakuna mipasho,
Hizi ni ngumu kwenye booth sokoni commercial
Hizi ni bum kubam, bu bu kubam kubum kubam, bubu kubam

Ubeti 2
Hapa nipo natoa maji kwenye kiu,
 sex figure Fatuma ndio chenyewe kiu
kiungwana mangaribi sara rescue, kata karateka Encarta is you,
nyie balloon kwenye parachute, wote ni puto nyie katuni kama penseli,
kichwa ufuto, platoon zinakuua kwenye booth now,
ukweli unakita kwenye chup waaaoh! Siwezi kiss kwenye mbingu naikiss ardhi,
ntashuka kwenye ardhi kuelekea mbingu, kifo cha mwenye haki honeymoon
bila kanisa kuna misa kwenye hali duni,
Naibuni rap, naitune swagga, mpo flat nyie si kama flat za maghorofani,
Mpo fat nyie si mpo slim kwenye fani, no one can try me m*@#$k you better run.

Kiitikio x 2
Nani anafyum uswazi hakuna mipasho,
Hizi ni ngumu kwenye booth sokoni commercial,
Hizi ni bum kubam, bu bu kubam kubum kubam, bubu kubam,

Ubeti 3 (G-nako)
Leo Punchline zinabatizwa kuwarudisha nyuma kwenye roots,
Niki pozi ni black (too black),
uswazi tunaishi kwa yeyo tuwe ma lords kwenye banks,
it’s like Bum kubam we call it bumbaks, na hizo ndio ala ngumu,
tamu kama ngararum kwa wachaga na push ndio warawararum,
kudumisha chama cha weusi kidumu, tunatumia muda mrefu kubuni,
wanachukua kiulanii hawa baboon, mangi si mangi duh,
wanasifiwa kwa swagga za kudu duplicate, ingiza tape kwenye deck,
press record na dial code kwa lawyer to communicate, yeah damn pilot,
twendeni kwenye market, I make record for the record check  crowd reaction,
and this is A city monster (Muungurumo wa simba)

 Kiitikio 
Nani anafyum uswazi hakuna mipasho,
Hizi ni ngumu kwenye booth sokoni commercial,
Hizi ni bum kubam, bu bu kubam kubum kubam, bubu kubam,


Friday, 4 January 2013

Hakuna Matata - Sugu

Sugu


kiitikio
Nataka swaga za hakuna matata,
Kama nataka flows pia hakuna matata,
Nataka peace, hakuna matata,
Kama unataka bifu pia hakuna matata,
Kama unataka flows pia hakuna matata,
Nataka peace, hakuna matata,
Kama unataka bifu pia hakuna matata
Hakuna matata, ha ha nha, hakuna matata, x2

Ubeti 1
Bado nachana kama na miaka ishirini, kuna time mpaka mwenyewe siamini
Kwenye hili game tulishakula yamini, so kuliacha haiwezekani,
Aibu kwao waliosema hatutaweza maana tumeweza,  tumeweza mpaka tumepitiliza
Kwa wana wote sitaacha kusisitiza, mambo yanapokuwa magumu kinachotakiwa kukaza,
Komaa kaza msuli, kumbkuka daima Mungu yu na mwenye kusubiri, nhaa
Sionekani sana Dar sababu naishi jimboni, kama sipo jimboni labda nipo mjengoni,
Daily ni barabarani, njiani, ndani ya landcruiser ama zoni,
kinachopunguza uchovu ndani na televisheni, watching CNN,

kiitikio
Nataka swaga za hakuna matata,
Kama nataka flows pia hakuna matata,
Nataka peace, hakuna matata,
Kama unataka bifu pia hakuna matata,
Hakuna matata haha ha hakuna matata, x2

Ubeti 2
Hakuna matata, lakini ukinigusa tu nakuletea utata,
Ndo maana mitaa ya kati wananiita mtata,
Kwa wanaonijua wengi wananikubali, na ndio maana sijali kama we haunikubali,
Kwani wanaonikubali wananitosha, Sugu anatisha, a.k.a baba Sasha,
Miaka yote maisha yangu ni kubisha, na inshallah ndoto zangu zote nitazikamilisha,
Mjengo mkali, wife mzuri, na Mungu kanijalia nna kabinti kazuri,
Na ingawa niko bungeni, bado ni mwananjeshi na Jenerali vitani,
Ukileta namna gani, jua nakupa namna gani,
Na sio sababu eti natembea na gun, bali sababbu wananiita president wa kitaani

Kiitikio x 2
Nataka swaga za hakuna matata,
Kama nataka flows pia hakuna matata,
Nataka peace, hakuna matata,
Kama unataka bifu pia hakuna matata,
Hakuna matata haha ha hakuna matata, x2

Outro
Sugu,
 na hii ni kwa mashabiki walikuwa wanaulizia track sio
One for the road, Deiwaka Baby

Wednesday, 2 January 2013

Nataka kulewa – Diamond

Diamond


Intro:
AM records!
Ayayayayaaaa we niache miye miye miye miye,

Ubeti 1
Uuusiniulize kwa nini, sababu utanizingua
Ukitaka jiunge na mimi, Kama ni pesa we kunywa ntanunua,
Mi mwanzo sikuamini, nikajuaga vya kuzua,
Kumbe mjinga ni mimi ninayetunza wenzangu wanachukua,
Ai, ooh mapenzi! Mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya,
Mie siwezi walionikuta waniache niseme jina, ooh mapenzi!
(Mapenzi) yalinifanya kama mtoto n ilie vibaya (Mapenzi)
Na nina mengi, yamenijaa moyoni

Kiitikio
Ooh nataka kulewa (lewa), nataka kulewa (lewa)
Nataka kulewa (lewa) zikipanda nimwage radhii
Nataka kulewa (lewa) mi nataka kulewa (lewa)
Nataka kulewa (lewa) zikipanda nimwage radhii
Aya ya ya ya we niache mie mie, mie mie x 2

Ubeti 2
Mi kwa mapenzi masikinii, nikamvisha pete kwa kumuoa,
Kukata vilimilimi vya wazushi, wanafki wanaompoonda,
Kumbe mwenzangu na mimi, ni bure tu najisumbua,
Si tuko kama ishirini, mabuzi, ving’asti wengine anawahonga,
Ai, ooh mapenzi! Mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya,
Mie siwezi walionikuta waniache niseme jina, ooh mapenzi!
(Mapenzi) yalinifanya kama mtoto n ilie vibaya (Mapenzi)
Na nina mengi, yamenijaa moyoni

Kiitikio
Ooh nataka kulewa (lewa), nataka kulewa (lewa)
Nataka kulewa (lewa) zikipanda nimwage radhii (tilalila)
Nataka kulewa (lewa, tilalila) mi nataka kulewa (lewa)
Nataka kulewa (lewa) zikipanda nimwage radhii
Aya ya ya ya we niache mie mie, mie mie x 2
Kulewa kulewa…


2030 – Roma ft Story

Roma Mkatoliki


Tanzania eeeh!
(Tongwe records baby)
nchi yangu ooooh!

Ubeti 1
Huwezi kuijenga Roma haikujengwa kwa siku moja,
Kwa Raha leo au samba mtoto, Tanga watakuja,
Hata Pancho pia ni Mwamba bado anakata viuno,
Kaskazini bila khanga ni Msondo bila Gurumo,
Alisema juu ya mwamba atalijenga kanisa,
Na halitatikisika,Waumini tuianze misa,
Kwenye njaa kula kuku aliyechinjwa na padre,
Walaaaah! Hadhana ikilia amka kamuombe Allah,
Bwa’ shee mrudie Mungu, Masanja kawa mchungaji,
Sujudu maka madina, tajiri hataki kuhiji,
Maulidi ubungo kibangu ndio mishahara ya madrasa,
Ona rafiki wa padre kawa muhasibu wa kanisa,
Tenda wanapeana kindugu, mwanangu kua uyaone,
Familia ilikata ringi na mama alibaki mjane,
Sikuwa na damu ya kiarabu kwamba ntayarithi mabasi,
Dingi hakutupa msingi, ona gari twaifanya taksi,
Tazama gongo la mboto, mtoto kamzaa mtoto,
Na atalelewa na nani baba yake mmemfunga keko,
Wape buku waue winga wale watoto wa Moroko,
Mungu atazidi kulinda, kesho utaiona sabato,
Mzee wa bandari kastaafu kajenga banda la uani,
Ana wake watatu, je watoto watarithi nini?
Ndio chanzo cha kurogana na kutupiana majini,
Huyu akimpandisha makata, Yule maimuna subiani,
Maana pesa ndo ilifanya tusiwe na tanga ndugu,
Pesa ilileta ubaguzi kati  ya Loyola na Pugu,
Pesa ndo ilichochea bifu ya Nice na Dudu,
Na pesa ndo ilimaliza vita ya Ruge na Sugu

Kiitikio
Tanzania eeeeh!
Mwanangu kua uyaone, kama ntawahi kuiona Paradiso mtunze mamako
Nchi yangu oooh!
Mwanangu kua uyaone, marehemu hufa na chake, pigana upate chako,
Tanzania eeeh!
Mwanangu kua uyaone, mwalimu cheza kibati wanao wasife njaa,
Nchi yangu ooooh!
Mwanangu kua uyaone, elimu imekosa thamani Necta imevuja kibaha,

Ubeti 2
Aminini nawaambieni, ujana ni maji ya moto,
Mtoto humzika mama, leo mama anamzika mtoto,
Ndo maana mama alisema nisimchumbie mmachame,
Mura shusha mapanga, naileta posa Tarime,
Bahari imechafuka, mpem ba iheshimu karafuu,
Hatari kama Nungwi, nahodha sio Kirikou,
Yakhee! Nirushie mtumbwi, mi mwamba sio kichuguu,
Hii ni vita ya msambaa, mbondei uditie maguu,
Ona kipindi cha bunge Dodoma inanuka ngono,
Spika akihairisha bunge, wengi watausapoti mgomo,
Wabunge mnadai posho muhonge dada zetu,
Kuna wanafunzi wa mama Salma vyuoni msicheze peku,
Wazanzibari hawaioni thamani ya huu muungano,
Ila kulichoma kanisa sio njia ya kuvunja agano,
Sioni sababu ya ubaguzi na kuua wasio na hatia,
Wakati alochanganya mchanga, mchanga umeshamfukia,
Muislamu gani unahonga bongo muvi mamilioni,
Mama anakufa mwaisela, kakosa dripu ya kwinini,
Ni heri ujenge msikiti tuitukuze mitume,
Anasa za bakulutu, unawatunza wacheza sebene,
Unamuheshimu Ramadhani, unazini mbele ya Shabani,
Kama ilishushwa Quraan, twendeni misikitini,
Anayedhihaki msaafu pengine kanisa halijui,
Sio kuchoma kanisa, ni kuuza bible Dubai,
Usihofu kumpoteza mmoja ili kumi waishi vema,
Watanzaia tunauoga, sio amani mnadanganywa,
Sacrifice for your son and daughter,
Amka ki fikra damu yako iwe chachu ya ukombozi dokta Ulimboka,
Mkinga usimuue mama ili uongeze kipato,
Utajiri upo kaburini, watu wamekufa na ndoto,
Leo Ridhiwani hafanani na Makongoro,
Dah! Sina hela ya kiroba, Rashidi nigongee ugoro,
Suka kaiangusha lori ya mafuta, yote ni magendo,
Waziri anaziuza pembe za ndovu na meno ya Tembo,
Nchi imejaa misitu, tuna uhaba wa madawati,
Tunakula vitu feki (what), TBS mko wapi?
RPC usitume kikosi ili uishushe Chadema,
Italipwa damu ya Mwangosi, Iringa semeni amina
Okoa wagonjwa wa saratani, mpakani zuia wakimbizi,
Kuliko kumwaga pesa kwenye tume za uchunguzi,
Muhimbili naumwa goti, eti dokta kapasua kichwa,
Mbeya wanapigwa nyundo ili raia wauze mabucha,
Amana wanatelekeza, watoto wanalia,
Mwananyamala wanatuua na hawaendi jela, jela anakwenda Kajala,

Kiitikio
Tanzania eeeh!
Mwanangu kua uyaone, jeshi acha kisirani gonga muhuri tuwaahi,
Nchi yangu oooh!
Mwanangu kua uyaone, Trafiki hasira za mkeo barabarani hazifahi
Tanzania eeeeh!
Mwanangu kua uyaone, wanahonga mashabiki ngoma zao hazirequest
Nchi yangu oooh!
Mwanangu kua uyaone, udini wa mapresenta, wapagani unatukosti,

Ubeti 3
Sauti hii itasikika mpaka Oldonyo Lengai,
Nikifa naomba nizikwe Tanga, na mje kwa shambalai,
You can kill me broo! But you can’t kill what I’m standing for,
Usiutamani urithi wa Baba, ikimshuka CD 4,
Tuzo sikustahili (Hahaaaaa) hii ni hatariii
Tuzo inachapa ya nani? (Kaizari) mpe kaizari,
Sio masaki, Ngara mtoni, mama anaiuza dadii,
Muziki umejaa stress kila nyumba ina msanii, (Oyooo)
Yanga wamemfukia mbuzi golini, Simba wanabundi,
Viongozi wanataka umate umate hawaujali ushindi,
Utasikia, Chuji kachujaaa! Kiburi choma mahindiii!
Kapigwa ligi ya jogoo, shahidi kamati ya ufundi,
Kijijini tupo wengi, mleteni daktari bingwa,
Anangoma utasikia, “anangoma twendeni kwa mganga,”
Pesa za kujikimu ndo ulichongesha kitanda,
Kulea mimba sio Mchezo, ba kijacho hujajipanga,
Profesa kanyimwa penzi, utasikia “Carol kadisko”
Na Carol analea ndugu kwa pesa ya bodi ya mikopo,
Pole mnaotafuta C, mwaka wan ne mnarisiti,
Huku Headmaster kaenda mjini, eti shule imeishiwa chaki,
Msiwaue wachimbaji wadogo, Geita inalia,
Kaburu umempa migodi, UDSM tuna injinia,
Unapewa kontena la Condoms, ili uihonge dhahabu,
MV spice ilipozama, TV inaonyesha taarabu!
Kamanga hawaiweki lami ili tuvukie Busisi,
Dereva usintoe kafara ili utimize hesabu ya bosi,
Sina cha kuweka rehani kwenye asasi za mikopo,
Bajeti ya kilimo kwanza, mkulima silioni soko,
Tanga mmekosa nini? Amkeni acheni umwinyi,
Hawa Wachaga hawatuwezi, ona manka bara ishirini,
Bandari chanu, Railway chali, Makamba iinue katani,
Zitto akiroga kasulu, si tunamrogea pangani,
Uchafu wa mrisho unafanya msafi aonekane benzi,
Sisadiki magazeti, waandishi wengi kanjanja,
Vijana ndio nguvu kazi, ila wengi wamejaa lutindi
Mitaani wamekata ringi,hadi friji wanaziweka bondi,
Majibu ya postmortem kashanunua wakili,
Na hakimu kapewa kiwanja Kimara apige kufuli,
Cheki dola nainunua, kesi napewa kapuku,
Mpole kama ngamia, mbele ya hakimu wa kisutu,

Kiitikio
Tanzania eeeeh!
Mwanangu kua uyaoneee
Nchi yangu ooooh!
Tongwe records baby!




Monday, 31 December 2012

Don’t cry - Makamua ft Saraha

Makamua


Makamua
Girl your heart know I like you, figure still to find what’s on ya mind,
At all night on waniweka roho juu dah! Girl you make me lose my mind

Saraha
Boy you’re the best and there is no one like you,
Kila mara nakuwaza wewe tu, mawazoni waniweka roho juu,
Boy you make me loose my mind

Makamua & Saraha
Nakwita njoo, mwili nafsi vyote visisite,
Come baby love unikumbate, after hugh nipe kiss,
Siku mingimingi baby nimemiss

Kiitikio
I don’t wanna se you cry, (heei eeiyo!)
I just wanna see you smilin’ (Heeei yeeiii)
Staki kuona ukilia, niliapa mwenyewe, (na na na na)
I don’t wanna see you sad eeh,
I just wanna see you smillin’ ( iyeee iyee)
Staki kuona ukinuna, niliahidi mwenyewe, ( na na na na)

Ubeti 2
Saraha
Lakini mpenzi tumeishi miaka mingi (Kwelii)
Uliniahidi tutakwenda kwa wazazi (Sawaa)
Nikuulizapo unasema nitoe wasiwasi (toa wasiwasi)
Moyo wangu upo kwako hebu nitoe wasiwasi, (nitakutoa wasiwasi)

Makamua
Kama tunda shelisheli, wanichizisha ki ukweli,
Mi nataka twende mbali, tuwe wote safarini,

Kiitikio
I don’t wanna se you cry, (heei eeiyo!)
I just wanna see you smilin’ (Heeei yeeiii)
Staki kuona ukilia, niliapa mwenyewe, (na na na na)
I don’t wanna see you sad eeh,
I just wanna see you smillin’ ( iyeee iyee)
Staki kuona ukinuna, niliahidi mwenyewe, ( na na na na)

Makamua
Tutakwenda kwa wazaziii ahhhaaaa aaa aaaaa
Namuahidi ka saraha (Saraha)

Kiitikio x 2
I don’t wanna see you cry, (heei eeiyo!)
I just wanna see you smilin’ (Heeei yeeiii)
Staki kuona ukilia, niliapa mwenyewe, (na na na na)
I don’t wanna see you sad eeh,
I just wanna see you smillin’ ( iyeee iyee)
Staki kuona ukinuna, niliahidi mwenyewe, ( na na na na)

Outro
 wakali kwanza x2 Saraha, makamua, Fundi Samweli...