Sunday, 4 August 2013

Majanga - Snura

Chombezo
Mo fire gal (Sauti ya kiume)

Beti 1
Mama yuko hoi mama tumpeleke hospitali,  Dokta anataka salary,
‘Pigwa nimepigwa mie, polisi kawai yeye,  kibao megeuziwa miye,
Mama yuko hoi mama tumpeleke hospitali, Dokta anataka salary,
‘Pigwa nimepigwa mie, polisi kawai yeye,  kibao megeuziwa miye,
Pombe nimenunua mie, kulewa kalewa yeye ugomvi kaanzisha yeye
Kijijini nimtoe mie, kumlisha nimlishe mie, jeuri afanye yeye
Pombe nimenunua mie, kulewa kalewa yeye ugomvi kaanzisha yeye
Kijijini nimtoe mie, kumlisha nimlishe mie, jeuri afanye yeye

Kiitikio
Majanga, majanga mbona majanga  x2

Majanga (Mbona mbonaaaaa) x3

Beti 2
Ndoa tumefunga sie mapenzi yetu wenyewe talaka udai wewe,
Nyimbo nimeimba mie, video nimeshuti mie, shoo ukafanye wewe,
Ndoa tumefunga sie, mapenzi yetu wenyewe, talaka udai wewe,
Nyimbo nimeimba mie video nimeshuti mie, shoo ukafanye wewe
Chumba nitafute mie, kodi nilipe mwenyewe, nje unilaze wewe
Gari ninunue mie, mafuta niweke, mie misele upige wewe
Chumba nitafute mie, kodi nilipe mwenyewe, nje unilaze wewe
Gari ninunue mie mafuta niweke mie misele upige wewe

Kiitikio
Majanga, majanga mbona majangaaaa x2

Majanga (Mbona mbonaaaaa) x3

Beti 3
Kumzaa nimzae mie, kumlea nimlee mi, matusi anitukane yeyee
Mahari atoe yeye, kuoa aoe yeye, vya ndani uvile wewe
Kumzaa nimzae mie, kumlea nimlee mi, matusi anitukane yeyee
Mahari atoe yeye, kuoa aoe yeye, vya ndani uvile wewe
Hela katafuta yeye, nyumba kajenga mwenyewe mali tugonmee sie,
Kufiwa nifiwe mie, kulia nilie mie pole uchukue wewe
Hela katafuta yeye, nyumba kajenga mwenyewe mali tugonmee sie,
Kufiwa nifiwe mie, kulia nilie mie pole uchukue wewe

Kiitikio
Majanga, majanga mbona majangaaaa x2

Majanga (Mbona mbonaaaaa) x3

No comments:

Post a Comment