Utangulizi
Dada tuma eeh! Ngoja kwanza,
Producer mbezi
Yo ha haaaa 0444
Ubeti wa 1
Picha linaanza kama muvi ya Solomoni,
Gafla vumbi linazidi wajanja wanavaa miwani,
Hii ndio dar karibu ili usijisikie nyumbani,
Hapo Ubungo usinunue simu utauziwa sabuni,
Panda daladala tukutane buguruni,
kuna watu wanapiga
ndole utadhania majini
Gizani usiku utaona rangi zote za bikini,
wanauza mwili ili wanunue wali maini,
usicheke broo! Kwa sababu mi sio Mr. Bean,
chunga wallet hapa kuna wizi wa mfukoni,
haukawii kushuka kwenye gari hauna phone,
kuwa makini uvukapo huku gari hazipigi honi,
dala dala zinaa,Bajaj zinakesha macho,
Kama huamini ngoja
siku ije uamini we Tomaso,
Wasio na kazi wanashindia stori za freemason,
Wajanja wamepanga sinza, Kino na Tabata,
Mchana wanazibua vyoo usiku wanakula bata,
Usikojoe ovyo bro! Mgambo watakukamata,
Hii ndio dar, mbona unadata kabla hata hujapata starter?
Kiitikio x 2
Mmh bata ni daily,
daily’
Karibu bushman kaa
chini tukupashe habari
Shangaa mataa Dar
ugongwe na gari (Dar es salaam ya sasa)
Ubeti wa pili
Karibu sana kwenye hili jiji la joto,
Uswahilini chumba kimoja baba mama na watoto,
Si ulisikiaga mabomu ya gongo la mboto?
Yalifanya rafiki yangu wa damu akafia Ghetto,
Yaliacha kovu kubwa kama la mbagala,
Dar es salaam watu wengi tu hawanaga pa kulala,
Kama unataka mirungi twen’ zetu mitaa ya ilala,
Magomeni, mi ujanja wangu wote niliitwa fala,
Watu wanaingiza pesa
wakiwa wamelala,
Watu wengi toka waje hawajawahi kurudi kwao,
Sababu hawana nauli japo wamemisi ndugu zao,
Kuhusu kushinda na njaa hapa ndo zao,
Wauza sura wanaishi kwa kuuza mademu zao,
Mama anauza bangi, Baba amekata ringi anashinda anacheza
bao,
Wake zao wanazini kulisha watoto wao,
Vijana wao wanatembeza karanga, wanatembeza maji,wanatembeza
vocha,
Jioni wanakabidhi hesabu kwa bosi wao,
Hii ndio dar, ukipenda unaweza kuiita bongo,
Machizi wakikosa hela ya bia wanakula gongo,
See, haiwi siri uswahilini ukipata mchongo,
Wapangaji watakuandama bro mpaka utahama,
Ni majungu mixer wanga, utaenda tu kwa mganga, U
tapo lala Ghetto kwako kasha ukamwagiwa mchanga
Kiitikio x 2
Mmh bata ni daily,
daily’
Karibu bushman kaa
chini tukupashe habari
Shangaa mataa Dar
ugongwe na gari (Dar es salaam ya sasa)
Ubeti wa tatu
Dar es salaam ingekuwa nchi, huku Rais angekuwa Lowasa
Huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa,
Usione watu wamependeza, wengine hawana hata mia,
Hapa mboga ni maharage, nyanya chungu na bamia,
Brother man anatembea toka keko kwa miguu,
Anakwenda mlimani city kununua mkate tu,
(Are you on the facebook?) Ndo maswali ya maduu,
Ukitaka demu wa peke yako kata mgomba lala juu,
Ukimwita demu wako bar wanakuja crew,
Utachunwa mpaka ubaki na raba ubaki miguu juu,
Hapa bomba halijatoa maji mwezi mzima,
Hii ni uswahilini tu na sio kwa jiji zima,
Twende Mbezi au Masaki yanatoka mwaka mzima,
Katiza Kwa Mtogole uporwe simu mchana,
Siku hizi mwanaume anavaa suruali ya kubanaa,
Siku hizi dada’ko anakalio za kichina, ukimtafuta humpati
Ameshakuwa wa kimjinimjini.
No comments:
Post a Comment