Wednesday 2 January 2013

2030 – Roma ft Story

Roma Mkatoliki


Tanzania eeeh!
(Tongwe records baby)
nchi yangu ooooh!

Ubeti 1
Huwezi kuijenga Roma haikujengwa kwa siku moja,
Kwa Raha leo au samba mtoto, Tanga watakuja,
Hata Pancho pia ni Mwamba bado anakata viuno,
Kaskazini bila khanga ni Msondo bila Gurumo,
Alisema juu ya mwamba atalijenga kanisa,
Na halitatikisika,Waumini tuianze misa,
Kwenye njaa kula kuku aliyechinjwa na padre,
Walaaaah! Hadhana ikilia amka kamuombe Allah,
Bwa’ shee mrudie Mungu, Masanja kawa mchungaji,
Sujudu maka madina, tajiri hataki kuhiji,
Maulidi ubungo kibangu ndio mishahara ya madrasa,
Ona rafiki wa padre kawa muhasibu wa kanisa,
Tenda wanapeana kindugu, mwanangu kua uyaone,
Familia ilikata ringi na mama alibaki mjane,
Sikuwa na damu ya kiarabu kwamba ntayarithi mabasi,
Dingi hakutupa msingi, ona gari twaifanya taksi,
Tazama gongo la mboto, mtoto kamzaa mtoto,
Na atalelewa na nani baba yake mmemfunga keko,
Wape buku waue winga wale watoto wa Moroko,
Mungu atazidi kulinda, kesho utaiona sabato,
Mzee wa bandari kastaafu kajenga banda la uani,
Ana wake watatu, je watoto watarithi nini?
Ndio chanzo cha kurogana na kutupiana majini,
Huyu akimpandisha makata, Yule maimuna subiani,
Maana pesa ndo ilifanya tusiwe na tanga ndugu,
Pesa ilileta ubaguzi kati  ya Loyola na Pugu,
Pesa ndo ilichochea bifu ya Nice na Dudu,
Na pesa ndo ilimaliza vita ya Ruge na Sugu

Kiitikio
Tanzania eeeeh!
Mwanangu kua uyaone, kama ntawahi kuiona Paradiso mtunze mamako
Nchi yangu oooh!
Mwanangu kua uyaone, marehemu hufa na chake, pigana upate chako,
Tanzania eeeh!
Mwanangu kua uyaone, mwalimu cheza kibati wanao wasife njaa,
Nchi yangu ooooh!
Mwanangu kua uyaone, elimu imekosa thamani Necta imevuja kibaha,

Ubeti 2
Aminini nawaambieni, ujana ni maji ya moto,
Mtoto humzika mama, leo mama anamzika mtoto,
Ndo maana mama alisema nisimchumbie mmachame,
Mura shusha mapanga, naileta posa Tarime,
Bahari imechafuka, mpem ba iheshimu karafuu,
Hatari kama Nungwi, nahodha sio Kirikou,
Yakhee! Nirushie mtumbwi, mi mwamba sio kichuguu,
Hii ni vita ya msambaa, mbondei uditie maguu,
Ona kipindi cha bunge Dodoma inanuka ngono,
Spika akihairisha bunge, wengi watausapoti mgomo,
Wabunge mnadai posho muhonge dada zetu,
Kuna wanafunzi wa mama Salma vyuoni msicheze peku,
Wazanzibari hawaioni thamani ya huu muungano,
Ila kulichoma kanisa sio njia ya kuvunja agano,
Sioni sababu ya ubaguzi na kuua wasio na hatia,
Wakati alochanganya mchanga, mchanga umeshamfukia,
Muislamu gani unahonga bongo muvi mamilioni,
Mama anakufa mwaisela, kakosa dripu ya kwinini,
Ni heri ujenge msikiti tuitukuze mitume,
Anasa za bakulutu, unawatunza wacheza sebene,
Unamuheshimu Ramadhani, unazini mbele ya Shabani,
Kama ilishushwa Quraan, twendeni misikitini,
Anayedhihaki msaafu pengine kanisa halijui,
Sio kuchoma kanisa, ni kuuza bible Dubai,
Usihofu kumpoteza mmoja ili kumi waishi vema,
Watanzaia tunauoga, sio amani mnadanganywa,
Sacrifice for your son and daughter,
Amka ki fikra damu yako iwe chachu ya ukombozi dokta Ulimboka,
Mkinga usimuue mama ili uongeze kipato,
Utajiri upo kaburini, watu wamekufa na ndoto,
Leo Ridhiwani hafanani na Makongoro,
Dah! Sina hela ya kiroba, Rashidi nigongee ugoro,
Suka kaiangusha lori ya mafuta, yote ni magendo,
Waziri anaziuza pembe za ndovu na meno ya Tembo,
Nchi imejaa misitu, tuna uhaba wa madawati,
Tunakula vitu feki (what), TBS mko wapi?
RPC usitume kikosi ili uishushe Chadema,
Italipwa damu ya Mwangosi, Iringa semeni amina
Okoa wagonjwa wa saratani, mpakani zuia wakimbizi,
Kuliko kumwaga pesa kwenye tume za uchunguzi,
Muhimbili naumwa goti, eti dokta kapasua kichwa,
Mbeya wanapigwa nyundo ili raia wauze mabucha,
Amana wanatelekeza, watoto wanalia,
Mwananyamala wanatuua na hawaendi jela, jela anakwenda Kajala,

Kiitikio
Tanzania eeeh!
Mwanangu kua uyaone, jeshi acha kisirani gonga muhuri tuwaahi,
Nchi yangu oooh!
Mwanangu kua uyaone, Trafiki hasira za mkeo barabarani hazifahi
Tanzania eeeeh!
Mwanangu kua uyaone, wanahonga mashabiki ngoma zao hazirequest
Nchi yangu oooh!
Mwanangu kua uyaone, udini wa mapresenta, wapagani unatukosti,

Ubeti 3
Sauti hii itasikika mpaka Oldonyo Lengai,
Nikifa naomba nizikwe Tanga, na mje kwa shambalai,
You can kill me broo! But you can’t kill what I’m standing for,
Usiutamani urithi wa Baba, ikimshuka CD 4,
Tuzo sikustahili (Hahaaaaa) hii ni hatariii
Tuzo inachapa ya nani? (Kaizari) mpe kaizari,
Sio masaki, Ngara mtoni, mama anaiuza dadii,
Muziki umejaa stress kila nyumba ina msanii, (Oyooo)
Yanga wamemfukia mbuzi golini, Simba wanabundi,
Viongozi wanataka umate umate hawaujali ushindi,
Utasikia, Chuji kachujaaa! Kiburi choma mahindiii!
Kapigwa ligi ya jogoo, shahidi kamati ya ufundi,
Kijijini tupo wengi, mleteni daktari bingwa,
Anangoma utasikia, “anangoma twendeni kwa mganga,”
Pesa za kujikimu ndo ulichongesha kitanda,
Kulea mimba sio Mchezo, ba kijacho hujajipanga,
Profesa kanyimwa penzi, utasikia “Carol kadisko”
Na Carol analea ndugu kwa pesa ya bodi ya mikopo,
Pole mnaotafuta C, mwaka wan ne mnarisiti,
Huku Headmaster kaenda mjini, eti shule imeishiwa chaki,
Msiwaue wachimbaji wadogo, Geita inalia,
Kaburu umempa migodi, UDSM tuna injinia,
Unapewa kontena la Condoms, ili uihonge dhahabu,
MV spice ilipozama, TV inaonyesha taarabu!
Kamanga hawaiweki lami ili tuvukie Busisi,
Dereva usintoe kafara ili utimize hesabu ya bosi,
Sina cha kuweka rehani kwenye asasi za mikopo,
Bajeti ya kilimo kwanza, mkulima silioni soko,
Tanga mmekosa nini? Amkeni acheni umwinyi,
Hawa Wachaga hawatuwezi, ona manka bara ishirini,
Bandari chanu, Railway chali, Makamba iinue katani,
Zitto akiroga kasulu, si tunamrogea pangani,
Uchafu wa mrisho unafanya msafi aonekane benzi,
Sisadiki magazeti, waandishi wengi kanjanja,
Vijana ndio nguvu kazi, ila wengi wamejaa lutindi
Mitaani wamekata ringi,hadi friji wanaziweka bondi,
Majibu ya postmortem kashanunua wakili,
Na hakimu kapewa kiwanja Kimara apige kufuli,
Cheki dola nainunua, kesi napewa kapuku,
Mpole kama ngamia, mbele ya hakimu wa kisutu,

Kiitikio
Tanzania eeeeh!
Mwanangu kua uyaoneee
Nchi yangu ooooh!
Tongwe records baby!




No comments:

Post a Comment