Wednesday, 2 January 2013

Nataka kulewa – Diamond

Diamond

Intro:
AM records!
Ayayayayaaaa we niache miye miye miye miye,

Ubeti 1
Uuusiniulize kwa nini, sababu utanizingua
Ukitaka jiunge na mimi, Kama ni pesa we kunywa ntanunua,
Mi mwanzo sikuamini, nikajuaga vya kuzua,
Kumbe mjinga ni mimi ninayetunza wenzangu wanachukua,
Ai, ooh mapenzi! Mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya,
Mie siwezi walionikuta waniache niseme jina, ooh mapenzi!
(Mapenzi) yalinifanya kama mtoto n ilie vibaya (Mapenzi)
Na nina mengi, yamenijaa moyoni

Kiitikio
Ooh nataka kulewa (lewa), nataka kulewa (lewa)
Nataka kulewa (lewa) zikipanda nimwage radhii
Nataka kulewa (lewa) mi nataka kulewa (lewa)
Nataka kulewa (lewa) zikipanda nimwage radhii
Aya ya ya ya we niache mie mie, mie mie x 2

Ubeti 2
Mi kwa mapenzi masikinii, nikamvisha pete kwa kumuoa,
Kukata vilimilimi vya wazushi, wanafki wanaompoonda,
Kumbe mwenzangu na mimi, ni bure tu najisumbua,
Si tuko kama ishirini, mabuzi, ving’asti wengine anawahonga,
Ai, ooh mapenzi! Mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya,
Mie siwezi walionikuta waniache niseme jina, ooh mapenzi!
(Mapenzi) yalinifanya kama mtoto n ilie vibaya (Mapenzi)
Na nina mengi, yamenijaa moyoni

Kiitikio
Ooh nataka kulewa (lewa), nataka kulewa (lewa)
Nataka kulewa (lewa) zikipanda nimwage radhii (tilalila)
Nataka kulewa (lewa, tilalila) mi nataka kulewa (lewa)
Nataka kulewa (lewa) zikipanda nimwage radhii
Aya ya ya ya we niache mie mie, mie mie x 2
Kulewa kulewa…

No comments:

Post a Comment