Friday 4 January 2013

Hakuna Matata - Sugu

Sugu


kiitikio
Nataka swaga za hakuna matata,
Kama nataka flows pia hakuna matata,
Nataka peace, hakuna matata,
Kama unataka bifu pia hakuna matata,
Kama unataka flows pia hakuna matata,
Nataka peace, hakuna matata,
Kama unataka bifu pia hakuna matata
Hakuna matata, ha ha nha, hakuna matata, x2

Ubeti 1
Bado nachana kama na miaka ishirini, kuna time mpaka mwenyewe siamini
Kwenye hili game tulishakula yamini, so kuliacha haiwezekani,
Aibu kwao waliosema hatutaweza maana tumeweza,  tumeweza mpaka tumepitiliza
Kwa wana wote sitaacha kusisitiza, mambo yanapokuwa magumu kinachotakiwa kukaza,
Komaa kaza msuli, kumbkuka daima Mungu yu na mwenye kusubiri, nhaa
Sionekani sana Dar sababu naishi jimboni, kama sipo jimboni labda nipo mjengoni,
Daily ni barabarani, njiani, ndani ya landcruiser ama zoni,
kinachopunguza uchovu ndani na televisheni, watching CNN,

kiitikio
Nataka swaga za hakuna matata,
Kama nataka flows pia hakuna matata,
Nataka peace, hakuna matata,
Kama unataka bifu pia hakuna matata,
Hakuna matata haha ha hakuna matata, x2

Ubeti 2
Hakuna matata, lakini ukinigusa tu nakuletea utata,
Ndo maana mitaa ya kati wananiita mtata,
Kwa wanaonijua wengi wananikubali, na ndio maana sijali kama we haunikubali,
Kwani wanaonikubali wananitosha, Sugu anatisha, a.k.a baba Sasha,
Miaka yote maisha yangu ni kubisha, na inshallah ndoto zangu zote nitazikamilisha,
Mjengo mkali, wife mzuri, na Mungu kanijalia nna kabinti kazuri,
Na ingawa niko bungeni, bado ni mwananjeshi na Jenerali vitani,
Ukileta namna gani, jua nakupa namna gani,
Na sio sababu eti natembea na gun, bali sababbu wananiita president wa kitaani

Kiitikio x 2
Nataka swaga za hakuna matata,
Kama nataka flows pia hakuna matata,
Nataka peace, hakuna matata,
Kama unataka bifu pia hakuna matata,
Hakuna matata haha ha hakuna matata, x2

Outro
Sugu,
 na hii ni kwa mashabiki walikuwa wanaulizia track sio
One for the road, Deiwaka Baby

No comments:

Post a Comment