Afande Sele |
Intro
Na na na na na na na naa na na na na naaa M-O-R-OOoh,
moro town yeah! Home sweet home x2 (uuh)
Ubeti wa kwanza -
Stamina
Chunga usipitilize stendi suka acha watu msamvu,
Moro imenipa mengi, washkaji pesa na shavu,
hatuna mpango na bahari, Mbona hata mindu ina fukwe,
Milima kwetu fahari, mwaka mzima kwetu full kipupwe,
Ausindile anoga ndio swagga za waluguru,
hata ufunge kwa kuroga ila Moro itaniacha huru,
sihitaji tena Baga utamu naupata Gairo,
Masai wote huu wana swagga karibu kama upo Njiro,
Toka enzi za Mbaraka mpaka wajukuu wa Mwinshehe,
Mkude kusimama Pastor, Mbokeleni kuwa sheikh,
Nina haki ya kujisifu, moro imenipa kitalu,
Namwaga Pombe kwa chifu wa Moro babu Kingaru,
Sina bifu na Mngoni, Mpogoro ndio napodeka,
Anzisha tifu ulingoni usande tukupe Cheka,
Mliotutoka kimwili Kiroho tupo pamoja,
Karibu Moro mswahili uzalendo uende kwa hoja,
(uuuuuh hu huuu)
Kiitikio
Karibu Morogoro, watu wote wa bara, visiwani mpaka Zanzibar,
Bahari sio kasoro, wageni karibuni hapa kwetu mtapata
furaha, x2
Urithi burudani vyote shwariiiiii, karibu mji kasoro,
Udzungwa ujionee ehee hee hee hee hee heee he mwenyewe,
Usisubiri usimuliweee, mwenyeweee (Yoo) Njooow
Ubeti wa pili – O - ten
Yeah! mji unaweza poa, niko rock juu mlimani,
Na mimi ndio mkuu wa mkoa karibuni madizini,
Matonya alifukuzwa Dar breki ya kwanza akaja shaini,
Mandela alikuwa shujaa, moro akaifanya maskani,
Si unajua? Miji kibao haipati mvua,
tofauti kubwa hapa kwetu inanyesha mpaka inaua,
Mzinga, Ndigutu,
Kichangani, Kiguru nyembe, hapa kwetu haina uzembe,
Hata star anashika jembe, Natokea matombo kilosa narudi
mzumbe,
Nampitia Mkude, makala yuko wapi Msinde,
Moro Bambam ila vichwa visivimbe,
narudi shamba hata muziki nisiimbe,
No, mi na moro tupo kama pacha,
yes karibu moro tuishi kama kacha,
Mbuga zipo na hata madini yapo,
palipo na amani ndo mi nilipo
Kiitikio
Ubeti wa tatu- Afande Sele
Morogoro,mjini kwetu,
Karibuni wote rafiki na ndugu
zetu(shua)
Toka pande zote iwe ndani, mpaka
nje ya nchi yetu,
Karibuni kwetu mtembeee, harakati
zetu mjionee,
Kama mimi na mtu chee, kuna
mashamba tunalimaga,
Mboga mboga na mipunga, kuna
mahindi, kuna matunda, viazi miwa na karanga,
Karibuni nyote Morogoro mchote,
hekima za Selemani mtangaze mataifa yote,
Mkawaambie, mlichokiona hapa,
mkawasimulie siri ya cheka kuwa chapa,
Na habari kibao za wakali wa
hapahapa, kwa soka kwa hip hop, ma streika marapa,
Maboxer, madensa wote waliotoka
hapa, wahapahapa, tangu kitambo kile,
Kabla ya Afande Sele, Kabla ya O
ten na Belle, kabla ya Supa Ngedere Moro Bado Chapa Ilale
Ngoma inogile, tuna historia tele,
hata mawlimu Nyerere alikuwaga Mbunge wa
Kwanza wa Moro miaka ile,
kwa wasiotambua hilo. Karibuni
Moro, hata tommorow
karibuni mjionee maajabu ya mzimu
wa Kolelo, ifakara Kilombero,
Tuliani, Mvomero, Kilosa na
Msowero, Masombo mpaka Gairo
Yeaaah hii ndio Morogoro mpaka
Nyachiro kwa mjomba Kobelo
Na Mahenge kwa shangazi wa
kipogoro, twende mahewaa
Kiitikio
Kibwagizo
Morogoro mji kasoro bahari kwetu
bado shwari
Morogoro, Mgeta Mzumbe Mlali Moro
imetulea
Nilipokula gimbi na kachumbari,
mwenzenu mimi naona fahari
Hata ninapokwenda mbali nitarudi
moro nyumbani
Nimelelewa angali bado kichanga,
bado mimi sijajua kuimba
Mpaka sasa mimi natamba, tena Moro
nimepata Mchumba mie x2
Nitazikwa Moro, Nitakufa Moro,
Naipenda Moro, nitaishi Moro
Kiitikio
No comments:
Post a Comment