Kala Jeremiah (Picha kwa hisani ya Bongo 5.com) |
Intro:
Rock town records,
Dear God let me talk to ya, cause am in the jungle,
I need your help, I
watch back and I see my self,
Yeah!
Ubeti
Asante Mungu leo ni siku nyingine,
Nakuja mbele yako baba leo nina ombi jingine,
Baba we ndo kimbilio sina tena mwingine,
Si unacheki sina furaha kama watu wengine,
Wanakula bata na kusaza zingine, Mimi bado niko ziro na
masela wengine,
Pengine labda umenisahau au umenichoka pengine,
Lakini hapana, we sio ka’ viumbe wengine,
Uliniumba wewe baba sio mtu mwingine,
Tena mimba yangu
ililelewa na baba mwingine,
Baba alikuwa bize na mademu wengine,
Nimeshamsamehe mwambie anamtoto mwingine,
Mwambie nampenda sana sina baba mwingine,
Mwisho wa yote mlaze mahali pema kama watu wengine,
Tukiachana na hayo nina mambo mengine,
Baba muziki wangu
ndio tatizo kubwa jingine,
Nachana sana promo wanapewa wengine,
Wengine wanasema niende kwa mganga pengine,
Lakini mi nimebatwizwa kama wakristu wengine,
Naijua biblia zaidi ya vitabu vingine,
Mungu wa Izraeli Mungu wa mataifa mengine,
Mungu wa Yakobo, Mungu wa Isaka, Mungu wa watu wengine,
Usikie kuomba kwangu nipe njia nyingine,
Naombea watoto mayatima na wenye shida wengine,
Wananchi masikini na tabaka jingine,
Mungu baba tupe neema
kama nchi zingine,
Watembelee mafisadi mmoja baada ya mwingine,
Wakumbushe kula kwa jasho kama watu wengine,
Ona mpaka nasahau mengine,
Baba ajira ziko chache hawapati wengine,
Vijana wanakula unga hawana kazi nyingine,
Dada zetu wanajiuza wengine,
Pengine labda ndo sodoma na gomora nyingine,
Wanaume siku hizi ni mashoga wengine,
Wanadai haiku zao kama haki zingine,
Wanaandamana
hadharani mataifa mengine,
Wanaoana kwa harusi kama ndoa zingine,
Tuachane na hayo masuala nina suala jingine,
Hivi ni kweli umewatuma manabii wengine?
Maana kila kukicha kuna kanisa jingine,
Huyu nabii, na huyu ni nabii mwingine,
Huyu anaponda na huyu anampinga mwingine,
Wanahubiri kuhusu pesa sio kitu kingine,
Toa ndugu toa, toa ulichonacho kingine,
Mungu nioneshe njia nioneshe ishara nyingine,
Yapo mambo mengi tu siwezi taja mengine,
Hata demu wangu nahisi anamshikaji mwingine,
Maana kabadilika kawa kama yule mwingine,
Niliyemfuma laivu akiwa na boya mwingine,
Nisamehe dhambi ya kuzini sina dhamboi nyingine,
Mwokozi wangu niongeze pesa zingine,
Rafiki zangu niongeze tena wengine,
Wawe wote wa ukweli sio ma-snitch wengine,
Wa kuchukua siri na kuvujisha kwingine,
Naomnbea madaktari waongezwe posho nyingine,
Ili usije kutokea mgomo mwingine,
Maana walikufa watu,
wasije wakafa wengine,
Mwisho wa yote nashukuru kwa uhahi mwingine,
Ninajua saa hizi watu wamelazwa wengine,
Rafiki zangu
walishagongwa na magari wengine,
Kama Farouk wa Lango na machizi wengine,
Mlaze pema Kanumba na rafiki wengine,
Tutaonana Yesu akirudi kwa mara nyingine,
Asante sana kwa baraza jingine,
Japo magamba yamevuka yakabaki mengine,
D classic moja inawatu wengine,
Wanadai nchi imeuzwa kwa jamaa mwingine,
Sajuki, Vengu na
wagoinjwa wengine,
Wanyooshee mkono wako wape afya nyingine,
Amin.
Kibwagizo – sauti ya
kike
Haleluya x 4
No comments:
Post a Comment