Wednesday 19 December 2012

Stamina ft Rich Mavoko - Kabwela

Stamina



Verse 1.
Nimepigwa msumari wa kichwa mwili unangoja kaburi,
Nimepiga picha nega zimetoka vivuli,
Dunia tambala bovu nalidekia kwa shida,
Najitahidi kuisolve bila kutumia four figure,
Natamani nisimame ili nione magharibi,
Moyo umejawa ukame, kuhema unajitahidi,
Macho yote yanaukungu utadhani chungu cha bibi,
Kumuomba Mungu shetani ananizidi spidi (Men)
Vizuri viko wapi, navisaka havionekani (dah)
Napata makapi vinono navitamani,
Sina baba, sina mama, sina babu, sina bibi,
Uchumi wangu umesimama kama behewa la itigi,
Umasikini unanipodoa bila kutumia cosmetics,
Daily unanizodoa unanivuta bila magnetics,
Maisha yangu hayana swaga kama mmasai wa njiro,
Natamani kula burger naishia viazi vya Gairo,

Chorus:
Leo nimepata kesho nimekosa,
Nachohifadhi maumivu tu, laifu ni ngumu bado inanichosha,
Nakula mbichi sili mbivu,
Uweza mimi bado ni kabwela, sina uhuru kama niko jela

Verse 2 
Kusoma kitajiri, kichwa kimejaa madufu,
Maisha hayana tafsiri usidhani yanamjua lufufu,
Naichora lami kwa mkaa kudhani ntaona chochote,
Class ningekaa, nisingeitwa Kiokote,
Pesa imegeuka Yuda, daily inanisaliti,
Mishale inazidi muda, utajiri unaninyima siti,
Maisha kama gwaride, Kuna wa mwisho na wa kwanza,
Yakisema nyuma geuka, wa mwisho anakuwa wa kwanza,
Taifa la kichwa changu Rais wake naona kichaa,
Na kitabu cha dhambi zangu kwa Mungu kimeshajaa,
Napatwa wazimu shida zinanitia madoa, Pesa imekuwa adimu kama Bikra kwa changudoa,
Banda nnalofugiwa sihemi halina dirisha,
Wasichana wananikimbia, wananiita nyoka wa kibisa,
Msosiwangu sio wa draft, sili mpaka nijitume
Maisha yana supa shafti yashanizidi nguvu za kiume.

Verse 3
Ushindi wangu ni uchafu, kwenye vita niwe safi,
Kila nnayemuomba tafu anataka nifanye  naye ulafi,
Maisha ni kombolela, maskini ndio mlinda kopo,
Cha msingi ni kuunga tela mapak ntoke kwenye msoto,
Jua linapozama natamani pasikuche, hasi inageuka chanya,
Kama kapeto anageuka sunche, naona alama ya mlango ila sioni pa kutokea,
Hii pesa imetoka jando inataka kunibabu Seya,
Nimegeuka konokono  natembea na mzigo wa shida,
Silali nimegeuka pono maishayanakwenda na mida,
Shida zishanipa ustaa zaidi ya kanda ya Loketo,
Nimezoea njaa hadi shibe naiona mseto,
Vikombe vya uaminifu nishavivunja mtaani,
Vijiko vy uhalifu nishaviweka kwenye sahani,
Mi nadhani haya maisha yana ramani,
 ila aliyewachorea masikini peni iligomea njiani

No comments:

Post a Comment