Friday, 28 December 2012

Mapito - Mwasiti ft Ali Nipishe


Mwasiti (Picha kutoka mtandaoni)

Mwasiti

Kosa kukueleza jinsi nnavyougua roho, moyo pendo hayaya,
Kama ungeelewa hili shamba lisingevunwa,
Mazao yanafanana  na  kijiji ulichokwenda, jinsia moja ila tofauti ni tabia
Aaaah aaaaah

Ali
Ndiwe unayenifanya usingizi nakosa,
Niwe unayefanya usiku nashindwa kulala

Mwasiti
Niwe unayenifanya mimi nashinda kuwaza
Niwe unayenifanya mapenzi nayaona machungu na kufumba macho

Ali
Hata nikilia, machozi yanaanguka chini
Hakuna wa kuyakinga wala yule wa kuyasitiri

Kiitikio – Mwasiti

Jua ni wewe uliyenipa ufalme wa mapito,
Acha nijute ukarimu wako na upole ndio chanzo
Jua ni wewe uliyenipa ufalme wa mapito
Acha niwaze, ukarimu wako na upole ndio chanzo,
Moyo roho hayaa aa

Kiitikio kinaendelea - Ali

Hata na mimi moyo roho hayaya

Ali

Nikikukosea , nakubembeleza huku nacheka,
Wanikumbatia sura kifuani umeilaza
Kumbe kwako moyoni unimanya kingasudadu na amwezi bwana x2

Mwasiti

Ungefumania, hata sura nisingenyanyua,
Sometimes I feel, bora nikaishi mbali,
mapenzi ni ya wawili jamaa,( eeh!)
moyo, roho hayayaaa

kibwagizo - Mwasiti

Niwe unayenifanya mimi nashinda kuwaza,
Niwe unayenifanya mapenzi nayaona machungu  na kufumba macho

Ali

Ni wewe baby, ni we kichuna changu
Ni wewe baby,
ni wewe x5
 kichuna changu

Kiitikio – Mwasiti     x2

Jua ni wewe uliyenipa ufalme wa mapito,
Acha nijute ukarimu wako na upole ndio chanzo
Jua ni wewe uliyenipa ufalme wa mapito
Acha niwaze, ukarimu wako na upole ndio chanzo,
Moyo roho hayaa aa

Ali

Hata na mimi moyo roho hayaya

1 comment:

  1. Utunzi maridadi japo kuna maneno machache nisiyoyaelewa. Kwa mfano
    1- Ufalme wa mapito ndio nini.
    2- Unimanya kingasudadu na amwezi bwana
    Kuna yeyote anayeweza kunipa maana ya semi hizi mbili.

    ReplyDelete