Ben Paul (Picha kwa hisani ya michuzijr.blogspot.com) |
Intro:
Huuuuu!
Ubeti 1
Hadithi ya penzi langu naikata nini mwisho,
Huthamini huoni pendo lako nalihitaji leo kesho,( Nshawahi kukosa?)
Mwenzenu nilisumbuka, mchana na usiku mimi (Nshawahi kukosa)
Nasema niliteseka, mchana na usiku mimi, (Nshawahi kukosa?)
Mwenzenu nilisumbuka mchana na usiku mi eeeh! (Sihitaji tenda kosa)
Najua nitateseka, mwisho sitakuwa nawe tena nauliza
Kiitikio x 2
Ni kama pete yangu inakuchoma kidoleni,
Ni kama pendo langu linakuchoma moyoni,
Bora kuitoa, aaah! Pendo kulivua
Bora kuitoa moyoni mwangu mi nisiteseke
Bora kuitoa, aaah! Pendo kulivua
Bora kuitoa moyoni mwangu mi nisiteseke
Ubeti 2
Sikujali wanafki walosema,
hatutadumu mimi na wewe tutaja achana,
wakiniona siko nawe si ndo watasema,
hata nyumbanii watajua tumefarakana,
Daraja
nikiwaza kwenda mbali, moyoni nahofia
maana bado nakujali,kwako nilishatua,
nikiwaza kwenda mbali, moyoni nahofia,
maana bado nakujali kwako nilishatua,
Ubeti 3
kila jema nitendalo (mie) kwako limekuwa siyo,
nitakapo kujua ulipo (mie) wanijibu utakavyo
pete kidoleni mwako, ya nisuta mwenzio,
ndio maana nikukosapo moyo wanienda mbio,
huuuuu yeeeeeh!
Kiitikio x 2
Ni kama pete yangu inakuchoma kidoleni,
Ni kama pendo langu linakuchoma moyoni,
Bora kuitoa, aaah! Pendo kulivua
Bora kuitoa moyoni mwangu mi nisiteseke
Bora kuitoa, aaah! Pendo kulivua
Bora kuitoa moyoni mwangu mi nisiteseke
Outro
Oooooho, mmmh classic sounds (Moni) aaaaah! New Ben Paul
(Sauti za miguno)
No comments:
Post a Comment