Rama Dee |
Ubeti 1
Utaambiwa sina
mapenzi
Utaambiwa si
mwaminifu mimi,
Utaambiwa sina
ubinadamu , kwenye mapenzi,
Utaambiwa sina
umuhimu kwako,
staili yangu si kuoa
ni ku cheat mademu, si kweli mpenzi
utaambiwa sina
mapenzi, ooooh!
Kiitikio
Jitahidi mpenzi kuwa
na subira,
Jitahidi mpenzi kuwa
na maamuzi, (true x2)
Juu ya penzi le,
pendo letu,x2
Ubeti - Mapacha
Hebu chukua maamuzi
we mjuzi mkufunzi,
Acha hizo ni makuzi,
upuuzi,
Jinsi naishi ni ka’
staa kwenye muvi,
Tumeshashea vingi
ukikataa ni mzushi,
Tuake chini ni balaa
ni uvumi,
Chuki tuliikataa
inayumbisha hadi uchumi,
Kumbuka furaha na
vitu vya msingi,
Madaha na majigambo
vitairudisha ligi, yes!
Rama Dee
Ukiambiwa mimi nipo
hata tu mtaani naganga naganga tu njaa,
Ukiambiwa mi muhuni,
sina kazi mama,
Kila nachopanga,
nachofanya juu yako mpenzi,
Kila niinalofanya,
ninalopanga ni juu yako
Kiitikio
Jitahidi mpenzi kuwa
na subira,
Jitahidi mpenzi kuwa
na maamuzi,
Juu ya penzi le,
pendo letu x2 (Maujanja saplaya)
Mapacha
Nasisitiza masimamo,
usiyumbishwe na maneno
Watu wengine
wanaongea midomo yao michafu,
Ukanihukumu ukaniona
kama mimi ni kavu,
Nna malengo juu yako
mimi si mpumbavu,
Upendo wa dhati
sintoonesha dharau,
Sikudanganyi hii
nataka ufahamu,
Mapenzi ya ukweli jua
uongo ni hatari,
Ahca tuwe na amani,
mawaki achana nao, yes!
No comments:
Post a Comment