Intro -Tunda
Ahaaaaaa ayeye yeeee
huuuuuuu
Pasha
Waswahili husema
mtoto umleavyo ndivyo akuavyo-oo,
Staki kuamini huu
usemi bora niache tu mambo kama yalivyo-oo,
Tunda
Shemeji nivipi hasa, kisa mkasa mpaka unalalamika
hivyo-o,
Nini kimekupata,
naona ka’ umedata sijakuzoea hivyo-o,
Pasha
Naona kwangu hili ni
balaa, binti anashinda tu baa,
Anakata kata tu
mitaa, huyu binti kiruka njia,
Tunda
Elewa Yule mtoto
washule, baa anatafuta visoda vya kufanyia tu hesabu-u
Shemu hemu punguza
ghadhabu, yeye ndo anazurura vipi anakuadhibu-u?
Pasha
Ananifanya nakosa
amani, wananicheka majirani,
Kila nakopitapita
mtaani vidole nanyooshewa mimi,
Ona mama yake
nilipomuoa, alikuwa na maadili mema,
Hata baba yake nimelelewa kwenye familia njema,
Tunda
Mtoto wa nyoka ni
nyoka, mi bado sijachoka atamfuta tu mama yake,
Huyu ado hajadondoka,
bado hajapotoka, atamfuata tu mama yake,
Kiitikio x2
Pasha
Wee shemeji
yangu,(shemeji yangu) bado tu hujajua,
Mbona mi nshatambua,
binti ameshakua, ha haaa
Tunda
Shemeji yangu mtoto
dunia inamzuzua, utoto unamsumbua,
Nakuahidi ataacha
akikua,
Ubeti 2
Pasha x2
Wiki nzima ndani
hajalala, kutwa anashinda kuzurura,
Hata sijui
anachokula, Mola atamlinda inshaalah,
Tunda
Wiki jana ye aliniga
kwamba anakwenda shule kujisomea,
Labda unalingine kwa
hilo jambo mi namtetea,
Ni kweli aliniaga
samahani shemu mi sijakwambia,
Naomba unambie kingine
ila kwa hilo unamsingizia,
Pasha x2
Hizo nguo zake ndizo
zinazo nichanganya mwenzenuuu,
Sina raha akipita
nilipokaa,
Hajali lolote hata
kama hiyo siku wamekuja wageniii,
Apotezea, she don’t
care natamani kuliaaa,
Kiitikio x2
Pasha
Wee shemeji
yangu,(shemeji yangu) bado tu hujajua,
Mbona mi nshatambua,
binti ameshakua, ha haaa
Tunda
Shemeji yangu mtoto
dunia inamzuzua, utoto unamsumbua
Nakuahidi ataacha
akikua
Kibwagizo
Pasha
Mtoto ameharibikaa x2
Mtoto ameharibika,
ameharibika, ameharibikaa
Tunda
Mtoto hajaharibika,
hajaharibiuka, hajaharibika x2
Pasha
Ona ameharibika x 2
Ona ameharibika,
ameharibika, ameharibikaa
Outro
Tunda
Huuuuuuu, yiiiiiiiiii
mmmh x3
Shebi fleva mwana,
Shebi fleva mwanangu, Shebi piga vinanda mjomba anaonewa sana
Shebi piga vinanda,
Shebi fleva piga vinanda, Shebi piga vinanda mjomba wangu anaonewa sana
Mmmmh! Mh mh mh Shei
fleva kiboko yao
No comments:
Post a Comment